Pages

Friday, July 5, 2019

HII NDIO PANGANI

                                           HABARI NA HISTORIA YA MJI WA PANGANI

Pangani


 ni moja ya wilaya inayopatikana katika mkoa wa Tanga. Wilaya hii inabeba historia ndefu sana kwenye nchi hii, Kwani Ni moja ya maeneo ya mwanzo kufikiwa na kukaliwa na Waarabu.Pangani ni miongoni mwa maeneo ya mwanzo ya Tanzania bara kufikiwa na wageni kuutoka mashariki ya kati miaka ya 600-900 ambao ndio hao Waarabu. Na hata kwenye miaka ya 1400, Pangani ni moja ya miji iliopata kufikiwa na Wareno. waarabu

Na hata vile vita kati ya Wareno na Waarabu Pangani vilifika na kuleta athari kubwa kwa jamii za mwazo za Wazigua. Lakini hata kwa upande wa Wabantu wa mwanzo kufika maeneo ya Pangani walifahamika kwa jina moja la Waseuta( habari zake zilishasimuliwa kwenye habari za Wazigua). 

Kihistoria kama inavyosimuliwa na wataalamu kama wakina Nkondokaya na wazee wa Tanga, wanasema kuwa mji wa Pangani ulianza kukua na kama unavyoonekana leo hii kuanzia miaka ya 1600/1700. Na mji huu ulipatwa kukuzwa na Wabantu ambao walikuwa wakifanya biashara na wageni kutoka mashariki ya mbali.

Na wakati mji huu unakuwa kulikuwa na maeneo ambayo yalipatwa kukaliwa na watu , maeneo hayo ni kama Hale, Maporomoko ya Muhembo na maeneo ya Mtindiro. Wanazidi kusisitiza kuwa mji huu wa Pangani wa sasa hivi ni mji wa sita kwani kabla ya hapo kulikuwa na miji mingine ambayo ilijengwa na kufa. Ukweli ni kwamba habari za mji wa Pangani zinajitoikeza hata kwenye vile vitabu vya masimulizi ya wasafiri kutoka Ugiriki( Periplus of Erythrean Sea). Na tunapozungumzia habari za masimulizi haya tunapata kusoma habari za mji wa zamani wa “Rapta” uliopata kuwepo miaka ya 80(BK au mb)

Kwa upande wa machifu na viongozi mbalimbali waliopata kujenga historia ya mji wa Pangani, wanatajwa wakina Zume Seif, Zumbe Mwera,Zume Upanga na Wakina Zumbe Zuberi. 
Asili ya jina hili Pangani linazua masimulizi mengi sana, hii inamaanisha kuwa kulizuka masimulizi mengi ambayo yalikuwa yanajaribu kusimulia asili ya jina Pangani. Kwa kumrejerea tena mwanahistoria Bwana Nkondokaya na masilimulizi niliyoyapata kutoka kwa watu wa Pangani, wanasema kuwa, asili ya jina Pangani linatokana na Pango au mapango yaliokuwa yakitumiwa na watu wa mwanzo kama makazi yao. 

Aidha neno hili pangani ni la kibantu lenye maana ya pangoni kwani asilimia kubwa ya watu waliokuwa wakiishi kwenye mapango.
Haikuishi hapo bado wanasema kuwa asili ya neno Pangani linahusiana na biashara ya utumwa. Kwani mji wa Pangani ni moja ya mji wenye historia kubwa ya biashara ya utumwa. Wanasema kuwa neno Pangani linatokana na neni la kiswahili Pangani. Kwani watumwa walikuwa wakiletwa katika pwani ya Pangani, walikuwa wakipangwa kwa lengo la kusafirishwa kwenye majaazi. Na hivyo watu wakaamua kupaita Pangani kama jina la sehemu ambayo watu hupangwa kabla ya safari za majini 

Kwa ujumla mji huu wa Pangani hasa kwa wakati huu ni moja ya sehemu za vivutio vya utalii nchini Tanzania. Kwani mji huu umehifadhi historia kubwa sana hapa nchini Tanzania tangu miaka ya 80 bf /af mpaka leo hii. Wilaya ya Pangani ina majengo mengi ya kale na yanatumika kama sehemu ya utaliiLeo hii pangani ni moya ya wilaya inayopatikana katika mkoa wa Tanga na wakazi wake wa asili ni wazigua hasa wale Waluvu, kutoka kwenye kundi la Waseuta. Hii ndio habari na historia fupi ya mji huu wa Pangani.









TAGAZA NASI SASA 
PHONE 0672990117

IFA HAMU HISTORY YA PANGANI

                                              IFAAMU HISOTY YA PANGANI



Ikilinganishwa na Tongoni,

Kaole na makazi mengine katika pwani ya Afrika Mashariki, Pangani ni makazi ya kisasa. Ilikua umaarufu katikati ya karne ya 19, wakati ulikuwa katikati ya sultanate ya Zanzibar na njia za msafara wa bara, na ilikuwa wakati huu wakati duka la mtumwa wa mto lilijengwa. Jengo la zamani zaidi la Pangani ni serikali ya zamani, ambayo ilifika mwaka 1810 na ilikuwa ni makazi ya kibinafsi ya mfanyabiashara wa tajiri wa Omani. Nyumba ya kisasa ya hivi karibuni, iliyojengwa miaka kumi baadaye. Pengine karne nyingi zaidi ni makazi katika Bweni, kinyume cha pande kinyume na Pangani kwenye benki ya kusini ya mto, ambako kaburi la karne ya 15 limepatikana. Mnamo Septemba 1888, Pangani ilikuwa mji wa kwanza wa kupinga utawala wa kikoloni wakati wa Uasi wa

Abushiri. Uasi wa Abushiri Ingawa Uasi wa Abushiri, mojawapo ya waasi wa kikoloni wa Afrika Mashariki, mara nyingi huhusishwa na Bagamoyo, Pangani ilikuwa mahali pa kuzaliwa kwake. Kichocheo kilikuja mwaka wa 1884, wakati Kijerumani mdogo, Carl Peters, alianzisha kampuni ya Ujerumani ya Afrika Mashariki (Deutsch-Ostafrikanische Gesellschaft au DOAG). Katika kipindi cha miaka michache ijayo, kwa jitihada za kuingiza biashara ya biashara ya misafara ya ndani ya nchi, Peters aliweza kupitisha makubaliano kutoka kwa Sultan wa Zanzibar kuwa DOAG inaweza kuchukua udhibiti wa ushuru wa forodha katika maeneo ya bara ya Sultan. Hata hivyo, mwakilishi wa Sultan wala Pani wala wengi wa wenyeji walikuwa na manufaa kwa wazo hilo. Wakati DOAG iliinua bendera yake iliyo karibu na ile ya sultani, mvutano wa kuchanganyikiwa ulilipuka. Chini ya uongozi wa mfanyabiashara wa Afro-Arabia aitwaye Abushiri bin Salim al-Harth, jeshi lililopangwa kwa ukatili, ikiwa ni pamoja na walinzi wengi wa Sultan, aliwafukuza Wajerumani, akiwashawishi mfululizo wa mapambano makubwa ya nguvu yaliyoendelea katika miji mingine ya bandari karibu na pwani . Wajerumani hawakushinda uasi hadi zaidi ya mwaka baadaye, baada ya kuwasili kwa reinforcements, kuimarishwa kwa blockade ya majini na kunyongwa kwa Abushiri. Baada ya uasi huo, DOAG ilifariki na mji mkuu wa kikoloni ulihamishwa kutoka Bagamoyo hadi Dar es Salaam.


WEKA MAONI YAKO JUU YA PANGANI

KWA MATANGAZO PIGA SIMU
0672990117

TEMBELEA YOTUBE YETU

PANGANI BRE
AKING NEWS TV




HII NDIO PANGANI

                                           HABARI NA HISTORIA YA MJI WA PANGANI Pangan i  ni moja ya wilaya inayopatikana katika mkoa w...